MKUU WA JKT AMSHUKURU RAIS NA AMIRI JESHI MKUU MAFUNZO YA JKT
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza mafunzo ya vijana wa JKT. Mkuu wa JKT amshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu mafunzo ya JKT. Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo leo tarehe 17 Aprili 2025 alipokuwa anahitimisha mafunzo ya Awali ya kijeshi kwa vijana wa Operesheni miaka 60 ya Muungano katika kikosi Cha Ruvu JKT kilichopo mlandizi mkoani Pwani. Amesema Malezi ni suala Mtambuka, yanaanzia ngazi ya familia, Vijana wanapofika makambini….


