SUMAJKT yatembelewa na Ugeni kutoka Comoros
Ugeni kutoka Kisiwa cha Comoro, tarehe 06 Septemba 23 umetembelea Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo Mlalakua jijini Dar es salaam. Ujumbe huo wa watu watano ukiongozwa na Mhe. Gavana Sitti Farouata Mhoudine umefika Makao Makuu ya SUMAJKT kwa ziara ya kikazi na umepokelewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Mhe. Gavana Sitti Farouata katika ziara hiyo amepata fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT kupitia Taarifa fupi iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa SUMAJKT. Luteni Kanali George Wang’ombe.Taarifa hiyo…


