WANANCHI WA COMORO WAFURAHISHWA NA BIDHAA KUTOKA SUMAJKT
Tarehe 12 hadi 19 mwezi Disemba 2022 kulifanyika Maonyesho ya Kibiashara eneo la ETG Moroni ambapo maonyesho hayo yaliratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro. Katika maonyesho hayo SUMAJKT ilialikwa kwa ujumbe rasmi wa balozi na uwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed. Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya serikali na wananchi wa nchi hizo mbili (Tanzania na Comoro) ambapo wananchi Comoro wafurahishwa na bidhaa kutoka SUMAJKT. Wananchi wa Moroni walipata fursa ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazozakishwa na SUMAJKT na wengi walionyesha kuridhishwa na viwango vya bidhaa hizo. Katika picha unaweza kushuhudia…


