Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.
JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz
Twendezetu Pace ya Kwata
Mapigano Na Mwendo
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.
JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz
Twendezetu Pace ya Kwata
Mapigano Na Mwendo
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa atuma salamu za Sikukuu kwa kuwatakia Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wa umma Heri ya Pasaka.
Waziri wa Ulinzi ambaye pia ni Katibu wa Rais nchini Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ikiwa ni Mwendelezo wa Mazungumzo ya kushirikiana katika biashara baina ya Shirika Hilo na Comoro. Mhe. Yousoufa akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania – Comoro Khalfan Saleh amepokelewa na Kanali Robert Kessy kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata Makao Makuu Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Ikumbukwe, ziara hiyo ya Mhe. Yousoufa Mohamed Ali imetokana na Makubaliano ya Awali ya kibiashara kati ya SUMAJKT na…
Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika. Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika. Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika…
Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu. Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na Askari kutoka Jeshi la Uganda (UPDF) wakiongozwa na Meja Jenerali Willium Nabasa, leo tarehe 29 Aprili 2025 wametembelea Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es Salaam ili kujifunza shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa na SUMAJKT kwa manufaa ya kuliendeleza Jeshi la Uganda. Maafisa hao wamepokelewa na Mkuu wa Shule ya Jitegemee Kanali Emmanuel Mwaigobeko, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizungumzia ugeni huo Kanali Mwaigobeko, amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na SUMAJKT. Jeshi la…
Tarehe 16 Januari 2023, Mkuu wa tawi la utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena alizindua magari 17 kwa ajili ya kuimarisha a utendaji wenye tija na kuboresha huduma za ulinzi. Aidha aliendelea kusema kwamba SUMAJKT itaendelea kutengeneza fursa mbalimbali kupitia kampuni ya SUMAJKT na hivyo kunufaisha Watanzania kwa ujumla. Bregedia Jenerali Hassan Mabena liendelea kuwashukuru na kuwaasa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuendelea kufanyakazi kwa kupitia kampuni tanzu za SUMAJKT.