Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation
Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation lililopo Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro kuanzia tarehe 11 Februari 2025.
Wawakilishi wa kampuni ya CAMPO ambao ni Prof Jamil Macedo ambaye ni Mtalaam wa Udongo pamoja na Bwana Cezar Rizzi Mtalaam wa Umwagiliaji wamewasili Nchini Tanzania Tarehe 10 Februari 2025 na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Kisha ugeni huo kuelekea Morogoro kutembelea Shamba ambalo awali liliitwa Kilombero Plantation Company Limited (KPL) na sasa SUMAJKT Mngeta Plantation kwa lengo la kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kilimo.




Kukamilika kwa Utafiti huo kutaongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na hatimaye kuchangia Usalama wa chakula nchini.
Pamoja na mchango wa Uzalishaji mazao, Wataalamu wa Utafiti na Ushauri wa Kilimo kutoka Kampuni ya CAMPO nchini Brazil wametembelea Shamba la SUMAJKT Mngeta Plantation ambapo Ziara hiyo inakuza Ushirikiano baina ya SUMAJKT na Taasisi mbalimbali Duniani katika Utafiti na Ushauri kwenye Sekta ya Kilimo na Biashara kwa ujumla.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube