JESHI la Kujenga Taifa (JKT) latangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo huku watakaopata nafasi hizo wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 Mwaka huu.

Akizungumza Septemba 25, 2024 na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT,Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Kanali Juma Mrai amesema usaili utaanza Oktoba 1, mwaka huu kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa kuja kujiunga ili kujengewa uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao” amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Amesema utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anatoka.

Ameongeza kuwa “ Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 mwaka huu ,aidha JKT linapenda kuwaarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira, wala kuwatafutia ajira kwenye asasi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali au vyombo vya ulinzi na Usalama” amesema.

Aidha amewaasa wazazi na walezi kujihadhari dhidi ya matapaeli ambao wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kutapeli wananchi kwamba wanaweza kuwasaidia kupata nafasi hizo kwa kutoa pesa ili wajiunge na JKT.

“Mara nyingi nafsi hizo zinapotangazwa wanaibuka matapeli ambao hudai nafasi hizo zinapatikana kwa kutoa fedha,naomba niwaambie nafasi hizo haziuzwi ni bure hivyo kila mmoja aombe sehemu husika zilizotolewa na JKT,”

Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

Similar Posts

26 Comments

  1. Form zakujiunga zinapatikana wapi? Nipotayari kujiunga naitwa Paul magele ni raia wa Tanzania Nina umri wa miaka 19 nipo kahama mkoa wa shinyanga mawasiliano 0687129714

  2. Makao makuu ya jkt,
    Bububu-Zanzibar.
    30/9/2024.
    Kwasheshima na taadhama naomba kupewa nafasi hii ya kujitolea kwaajili yakuijenga nchi yangu na kujijenga Mimi mwenyewe kuwa mkakamavu na shupavu katika kujipambania mimi mwenyewe na nchi yangu na naahidi kuweza kuhimili mazoezi yote na mafunzo yote nitakayo pewa .
    Asante

  3. Nashukuru Mungu kwa kuwa mmefanya jambo zuri na la kupendeza nawapongeza sana jeshi la kujenga taifa, kwa kukutazamia sisi vijana niwape pongezi na hongera maana pia ni sehemu ya ndoto zangu kulijenga taifa, hivyo natumaini hata maombi yangu yatakubalika, Asante.

  4. Kwa majina naitwa charles fredy komba nina umri wa miaka ishirini lakini nilikuwa na maoni yangu kuw sisi vijana wenye umri wa miaka ishirini na siku kadhaa ..tunakataliwa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa kwa kigezo cha kuwa tumezidi siku katika hiyo miaka ishirini hivyo ninaomba na sisi tulio na miaka ishirini na siku kadhaa tupewe fursa…kwan naipenda nchi yangu.

  5. Napenda kulitumikia jeshi la nchi yangu mkinipa nafasi nitalitumikia kwa moyo wote na kwa nguvu Zang zoto

  6. Yah maombi ya jeshi lakujenga taifa jkt mimi kihele Ezikieli Balihali nikijana wa kitanzania mwenye umuli wa myaka 18 pia nimwanye mafunzo ya jeshi la hakiba nimehitimu wilaya ya busega mukoa wa simiyu hinyo nikijana mwenye utimilifu wa kijeshi la hakiba pia nimwenye nizam na uhodali katika kazi hivyo naamini maombi yangu yatakubaliwa kujiunga na jeshi la kujenga taifa la jkt hivyo naambatanisha baluwa hii na nakala ya vyeti vyangu kama ifatavyo 1 cheti cha kuzaliwa namba 2 cheti cha kumaliza dalasa la saba 3 cheti cha kuhitim mafunzo ya jeshi la hakiba 4 utambulisho wa nidaa wako katika ujenzi wa taifa / Asante namba yang 0780838612

  7. Kwa majina naitwa Gabriel kitara waryoba ni mtanzani mzalendo mwenye umri wa miaka 21 nimemalza kidato Cha sita 2024 shauku yangu kubwa ni kujiunga na jeshi la Tanzania.tafadhal nahitaji msaada wetu

  8. Athuman Sudi Athuman says:
    October 7, 2024 at 3:59 pm

    Habari za wakati huu viongozi kwa majina naitwa ATHUMAN SUDI ATHUMAN nimzaliwa wa Tanzania Mkoa wa Shinyanga Wilaya ya Kahama Kata ya Isaka ni mezaliwa mwaka 2005 ninaumri wa miaka 19 ninaomba kujitolea kwa ajili ya kujenga na kuimalisha ulizi wa Tanzania pamoja na jeshi lake nipo tayari kujiunga na kula kiapo kwa ajili ya Tanzania natumai maombi yangu yatajibiwa Asanteni mwenyezi mungu awajalie muwe na siku njema

      1. Et muda wakupokea barua za maombi umeisha? Maana walinzi wa pale office ya mkuu wa wilaya wanakataa mm kupeleka

  9. Naitwa Japhet mipawa naishi mkoani lindi nahitaji kujiunga na mafunzo ya jeshi jkt Tanzania Mimi ni mtanzania namba yangu 0742369284

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *