|

Brigedia Ngata azindua magari ya Usafi SUMAJKT

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua magari matano yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni moja ya Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) Kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele.

Akizindua magari hayo Leo tarehe 19 Novemba 2024, Brigedia Jenerali Petro Ngata ameeleza kuwa Menejimenti ya SUMAJKT imejiwekea mikakati ya kuendelea kuongeza vitendeakazi ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT, Kapteni Rosemary Katani amesema kuwa Kampuni hiyo inatoa huduma ya usafi katika mikoa yote Tanzania Bara na hadi sasa imefanikiwa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 1600.

Kampuni ya Usafi na Unyunyizi Dawa ya SUMAJKT inafanya kazi katika Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na watu Binafsi.

Similar Posts

  • SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi

    SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi. Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) imezidi kujiimarisha kwa kununua mashine za kisasa za kufagia barabara ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Taasisi na Kampuni mbalimbali nchini. Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, leo tarehe 30 Aprili 2025 baada ya kuzindua Mashine za kisasa za kufagia barabara amewahimiza watendaji wa kampuni hiyo kutunza mashine hizo ili ziweze kuleta tija kwa shirika. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua uwepo wa Mashine hizo kutaiongezea kampuni hiyo uwezo zaidi…

  • Waziri wa Ulinzi Angola, aridhishwa na shughuli za SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT). Akizungumza baada ya kufanya ziara SUMAJKT leo tarehe 11 Januari 2025, Mhe. Dos Santos, amebainisha kuwa amevutiwa na uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo, hivyo wataenda kufanyiakazi nchini kwao. “Wizara yetu ya Ulinzi nchini Angola kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania tutakuja kusaini hati ya awali ya makubaliano ambayo itaonesha maeneo ya kushirikiana” alisema Mhe. Dos Santos. Aidha, Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania kupitia JWTZ kwa kuwezesha…

  • Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT

    Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amepokea ugeni wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka nchini Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi, ambaye amefanya ziara Makao Makuu ya SUMAJKT ili kubadilishana uzoefu katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo. Ugeni huo baaba ya kupokelewa leo tarehe 28 Aprili 2025 umetembelea Kiwanda cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi na Mradi wa SUMAJKT Energies ili kujionea shughuli za…

  • Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT

    Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu Nchini Namibia Meja jenerali Aktofel Nambahu Amevutiwa na Shughuli za Uzalishaji mali zinazofanya na Jeshi la Kujenga Taifa Kupitia Shirika lake SUMAJKT. Meja Jenerali Nambahu amepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele leo tarehe 20 Agosti 2025 Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT. Ziara yangu JKT ni mualiko wa Mkuu…

  • Meja Jen. Mabele aikaribisha SUA Makao Makuu ya JKT Dodoma.

    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa. Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho. Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo…

  • Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT

    Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT. Ugeni wa Wakufunzi na wanafunzi chuo Cha Taifa Cha Mafunzo ya Usalama nchini Nigeria wafurahishwa na Shughuli za Jeshi la Kunega pamoja na Shirika lake SUMAJKT. Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 25 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara huo Makamu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo Bwana Hyginus Ngele Umepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa jijini Dar es salaam tarehe…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *