Shule ya Jitegemee JKT yatimiza miaka 50, Jenerali Mhona atia neno

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Michael Muhona ameipongeza Shule ya Sekondari Jitegemee JKT kwa kutimiza Miaka 50 Tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza katika Sherehe ya Maadhimisho hayo zilizoambatana na Harambee maalaumu ya kuchangia maboresho ya Shule hiyo Meja Jenerali Muhona amesema JWTZ linaunga mkono dhamira ya Mageuzi inayofanyika, huku akitoa wito kwa walimu kuhakikisha Shule inaendeleza viwango bora vya Ufahulu.

Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Jitegemee JKT kilifanyika tarehe 01 Novemba 2024 ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT.

CHANGIA ELIMU KWA MABORESHO YA MIUNDO MBINU
1.NMB….23610041922
2.CRDB…0150892958700
3.LIPA….22426113 TIGO.
4.LIPA….54359412 VODACOM
Majina ya akaunti zote ni “JITEGEMEE (JKT) SECONDARY SCHOOL “

Mawasiliano:
+255755874191
+255717286100

Taarifa zaidi tumekuwekea kwenye chaneli yetu ya Youtube hapa chini..

Similar Posts

  • BRIGEDIA SHIJA LUPPI ATEMBELEA SHOWROOM YA SUMAJKT FURNITURE COMPANY

    Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Shija Lupi, ametembelea Eneo la Mauzo (Show room) la Kampuni ya Samani (SUMAJKT Chang’ombe Furniture Co.Ltd) lililopo karibu na Barabara ya Mwai kibaki Mlalakuwa Jijini Dar es salaam, tarehe 01 Disemba 2025 ili kuona Mwenendo wa biashara unavyoendelea. Brigedia Jenerali Lupi amepokelewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Meja Hemed Mchwanga ambapo amemueleza kuwa Kasi ya wateja kununua Samani zinazozalishwa na Kampuni ya SUMAJKT imeongezeka mara dufu katika kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka. Kampuni ya Samani ya SUMAJKT imeendelea kuzalisha bidhaa Bora na…

  • Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta

    Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema shirika lina dhamira ya kuendelea kujitanua na kuimarisha miundombinu ya kimkakati ya biashara ikiwemo sekta ya nishati. Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema hayo katika uzinduzi wa gari la kusafirishia mafuta la Kampuni ya SUMAJKT Logistiki leo tarehe 26 Mei 2025, Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT azindua gari la kusafirisha mafuta. Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua gari hilo litaongeza ufanisi katika usambazaji wa nishati ya…

  • SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga….

  • MAAFISA JKT WAMEASWA KUTEKELEZA KWA WELEDI JUKUMU LA MALEZI YA VIJANA

    Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana. Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa…

  • |

    SUMAJKT Electric Co Ltd kuwasha umeme vijiji 51 wilayani Kishapu, Shinyanga.

    Zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, mkoani Shinyanga huku vijiji vitatu vikiwashiwa pia huduma ya umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja. Mkandarasi SUMAJKT Electric Co Ltd ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanzakusambaza huduma za umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali. Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amepongeza kasi ambayo SUMAJKT Electric Co Ltd wameanza nayo ya kusambaza…

  • |

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu

    Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu. Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na Askari kutoka Jeshi la Uganda (UPDF) wakiongozwa na Meja Jenerali Willium Nabasa, leo tarehe 29 Aprili 2025 wametembelea Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es Salaam ili kujifunza shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa na SUMAJKT kwa manufaa ya kuliendeleza Jeshi la Uganda. Maafisa hao wamepokelewa na Mkuu wa Shule ya Jitegemee Kanali Emmanuel Mwaigobeko, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele. Akizungumzia ugeni huo Kanali Mwaigobeko, amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na SUMAJKT. Jeshi la…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *