SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo.

Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam.

Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga.

Kikao cha Wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania hufanyika kwa ajili ya kujadili namna ya kuboresha Uzalishaji na kuongeza tija katika mashirika hayo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *