Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT
Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi hao watatembelea Viwanda vya Shirika vilivyopo eneo la Mgulani JKT Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube.