SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi

SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi. Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa (SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd) imezidi kujiimarisha kwa kununua mashine za kisasa za kufagia barabara ili kuendelea kutoa huduma bora kwa Taasisi na Kampuni mbalimbali nchini.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, leo tarehe 30 Aprili 2025 baada ya kuzindua Mashine za kisasa za kufagia barabara amewahimiza watendaji wa kampuni hiyo kutunza mashine hizo ili ziweze kuleta tija kwa shirika.

Aidha, Brigedia Jenerali Ngata, amefafanua uwepo wa Mashine hizo kutaiongezea kampuni hiyo uwezo zaidi wa kutoa huduma kwa ufanisi.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co.Ltd Kapteni Athuman Msangi, ameeleza mashine hizo aina ya SP4 zitarahisisha kazi za usafi wa barabara.

Uongozi wa SUMAJKT umekuwa ukifanya jitihada za dhati kuhakikisha kampuni zake tanzu zinakuwa na vitendea kazi vya kutosha ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. SUMAJKT Cleaning and Fumigation yajiimarisha kisasa kwenye usafi.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *