“The Home of Quality Products and Services.”

Karibu SUMAJKT

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya mashirika ya umma ya mwaka 1974 (iliyorekebishwa mwaka 2002) baada ya amri ya Rais ya mwaka 1982. Shirika lilianzishwa ili kusaidia miradi ambayo ina uwezo mkubwa wa uzalishaji ili iweze kuzalisha zaidi na kwa faida na hivyo kusaidia serikali katika kupunguza matumizi ya kuendesha shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa.

Neno la CEO

“Ndani ya miaka 41 tangu kuanzishwa kwake SUMAJKT limeendelea kujipambanua kipekee katika ujenzi wa Taifa kupitia malezi ya vijana wa Taifa letu, uwekezaji katika sekta za Kiuchumi, Huduma katika Jamii na Uchangiaji katika pato la Taifa. Ili shirika liwe endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae, tunaamini katika Ubunifu, Uadilifu, Uwajibikaji, Ufanisi na Weledi kuwa ni msingi imara katika kutimiza Dira na Dhima ya kuanzishwa kwa SUMAJKT.”

  • Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT.

Washitiri wetu

Dira ya Shirika

“Kuwa shirika Kubwa, lenye sifa kibiashara na litakalokuwa na uwezo wa kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuendesha shughuli zake.”

Jengo la Kitega uchumi la SUMAJKT lililopo eneo la Medeli, jijini Dodoma

Dhima ya Shirika

“Kuanzisha na kuendesha shughuli za uzalishaji mali na huduma kwa tija katika sekta za Ujenzi, Viwanda, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji na sekta ya Biashara na Huduma. Pia shirika linajikita kutoa huduma kwa ufanisi, ubora na weledi.”

UBUNIFU

UADILIFU

UFANISI

WELEDI

Jengo la Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

SUMAJKT IPO KWA KUHUDUMIA KILA MWANANCHI

makampuni tanzu

miradi ya shirika

wateja

1982

kuanzishwa

Ungependa kuuliza swali?

Jaza formu hii tafadhali!

Karibu Ofisi zetu Makao Makuu SUMAJKT, Mlalakua, Dar es Salaam.

“The Home of Quality Products and Services.”