Similar Posts
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT. Mkuu wa Tawi la Mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Longinus Nyingo tarehe 16 Aprili 2025 amekagua Maandalizi ya Mwisho kuelekea kuhitimishwa kwa zoezi la Ufungaji wa Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano katika Kikosi cha Ruvu JKT Mlandizi mkoani Pwani. Kanali Nyingo amesema kuwa, zoezi la ufungaji wa Mafunzo katika Vikosi vyote vya JKT lilianza tarehe 8 Aprili 2025 ambapo Mkuu wa JKT alikuwa akiwakilishwa na Wakuu wa Matawi…
Meja Jen. Mabele aikaribisha SUA Makao Makuu ya JKT Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa. Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho. Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo…
SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba
SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam. Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam. Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT…
Brigedia Jenerali Petro Ngata apokelewa kwa Furaha SUMAJKT
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa Brigedia Jenerali Petro Ngata, amepokelewa kwa furaha na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Brigedia Jenerali Ngata akipokelewa kwa mara ya kwanza tangu apandishwe cheo hicho kutoka cheo cha Kanali, alianza kukaribishwa kwa gwaride la heshima na baadae kupokelewa na kamati ya Utendaji ya SUMAJKT. Akizungumza katika ukumbi wa mikutano Brigedia Jenerali Ngata ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu Meja Jenerali Rajab Mabele…
CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.
CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda, amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa maono ya kuanzisha Kampuni ya Bima ya Maisha (SUMAJKT Life Insurance Co. Ltd) itakayokuwa Msaada mkubwa kwa Watanzania kwa Vizazi vya sasa na Vijavyo. Jenerali Mkunda, ameyasema hayo Tarehe 10 Mei 2025 katika Sherehe ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Maisha ya SUMAJKT tukio lililofanyika Ukunbi wa (The Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam. CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Amesema imani yake ni kuona watanzania wakipatiwa huduma hiyo ya Bima kwani Jeshi…
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu. “Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi…


