Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.
JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz
Twendezetu Pace ya Kwata
Mapigano Na Mwendo
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.
JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz
Twendezetu Pace ya Kwata
Mapigano Na Mwendo
DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…
Washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Mataifa 16 Duniani wamefanya ziara ya Kimafunzo Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma mnamo Machi 10, 2025. Wakiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wamepata wasilisho la Namna JKT na Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) linavyotekeleza majukumu yake ya Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi. https://www.instagram.com/p/DHBmQZOIPxl/?igsh=cXZmNjdhZGp1ZDFw Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu. “Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi…
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa atuma salamu za Sikukuu kwa kuwatakia Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wa umma Heri ya Pasaka.
Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT, imewasili Jijini Tanga hi tarehe 10 Novemba 2024, kwa ajili ya kushiriki Michuano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA) iliyoanza Kutimua vumbi katika jiji hilo. Akizungumza mara baada ya kuwasili Jijini Tanga Katibu wa Kamati ya SHIMMUTA Kapteni Kichawele Bokassa, amesema timu imejiandaa vizuri kushiriki Michuano hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Albert Chalamila ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zilizopo Dar es Salaam kuhakikisha wanafika kiwanda cha SUMAJKT Skyzone kilichopo Mlalakua jijini hapo ili kutoa oda za kutengeneza taa bora za barabarani. “Tumepita tumeona teknolojia ya kiwanda hiki., naomba nitoe neno rasmi.., wakurugenzi wote wa halmashauri za Dar es Salaam, kufanya ziara mara moja katika kiwanda hiki, na ikiwezekana kutoa oda za taa.., ili ziweze kufungwa kwenye mji wetu kuhakikisha mji unafanya kazi masaa 24.” Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema kwamba Kiwanda hiko ni cha kwanza kabisa kwa aina…