|

SUMAJKT Electric Co Ltd kuwasha umeme vijiji 51 wilayani Kishapu, Shinyanga.

Zoezi la uzinduzi wa kuwasha umeme limefanyika Februari 17, 2023 wilayani Kishapu, katika Kijiji cha Itilima Shule ya Msingi Isunda, mkoani Shinyanga huku vijiji vitatu vikiwashiwa pia huduma ya umeme ambavyo ni Itilima, Ikonokelo na Ipeja. Mkandarasi SUMAJKT Electric Co Ltd ambaye anatekeleza mradi wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa Pili wilayani Kishapu na Shinyanga, ameanzakusambaza huduma za umeme katika Vijiji, Kaya na Taasisi za Serikali.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme wilayani Kishapu kwa vijiji hivyo vitatu, amepongeza kasi ambayo SUMAJKT Electric Co Ltd wameanza nayo ya kusambaza umeme kwa wananchi na taasisi za Serikali, na kuwaomba waendelee na kasi hiyo hiyo ili kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 wilayani humo viwe na huduma ya umeme.
“Shukrani SUMAJKT naomba muendelee na bidii ya kuunganisha umeme kwa wananchi na Taasisi za Serikali na ikifika Agosti vijiji vyote 51 wilayani Kishapu viwe na umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” amesema Mkude.


“Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha na kutekelezwa miradi hii ya umeme vijijini ambacho kilikuwa kilio cha wananchi kwa muda mrefu lakini ndani ya utawala wake wa miaka miwili wananchi wa Kishapu wanapata umeme na leo tumewasha katika vijiji vitatu,” ameongeza Mkude.


Naye Meneja wa Shirika la ugavi wa umeme Tanzania mkoani Shinyanga (TANESCO) Mhandisi Leo Mwakatobe, amesema Shirika hilo litapeleka wataalam kwenye vijiji hivyo vilivyounganishiwa Nishati ya umeme ili kutoa elimu kwa wananchi na wajiunge kwa wingi kuunganishiwa huduma hiyo.


Meneja wa TANESCO wilayani Kishapu Mhandisi Elias Turnbull, amewaonya wananchi ambao tayari wana Nishati ya umeme kijijini kwao, wasije wakatumia vishoka kuunganisha umeme kwenye Kaya zao bali watumie wataalam kutoka TANESCO.


Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema amefurahishwa na kasi ya usambazaji umeme katika vijiji wilayani Kishapu, na kuwaomba wananchi wasihujumu mradi huo na kuiba miundombinu yake na kuiingiza hasara Serikali, huku akiwataka viongozi na Jeshi la Jadi Sungusungu kuhakikisha ulinzi unaimarika ili usifanyike wizi wowote wa vifaa.


Aidha, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya umeme kutoka SUMA JKT Major James Mhame, amesema kwa kasi waliyonayo ya kusambaza umeme vijijini wilayani Kishapu kwamba hadi kufikia Agosti mwaka huu vijiji vyote 51 vitakuwa na huduma ya Nishati ya umeme, pamoja na wilaya ya Shinyanga vijiji 50 ambapo huko kampuni ya SUMAJKT Electric Co Ltd tayari wameshawasha umeme
vijiji 10, Kishapu vijiji vitatu na wiki ijayo watawasha tena vijiji vingine.


“Kasi tuliyonayo ni nzuri tayari tumeshapokea nguzo za
umeme 400 na zinakuja tena zingine 6,000 tunamuahidi
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hatutamwangusha kwa
kutuamini sisi SUMAJKT na kutupatia kazi hii ya
kusambaza Nishati ya umeme vijijini na tutamaliza ndani
ya muda,”amesema Meja Mhame.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Itilima Mkwaya Mwandu, amesema kupata huduma hiyo ya Nishati ya umeme Kijijini humo itachochea fursa za kiuchumi, na kuipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi huo wa umeme wa REA vijijini.

Similar Posts

  • Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT

    Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amepokea ugeni wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka nchini Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi, ambaye amefanya ziara Makao Makuu ya SUMAJKT ili kubadilishana uzoefu katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo. Ugeni huo baaba ya kupokelewa leo tarehe 28 Aprili 2025 umetembelea Kiwanda cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi na Mradi wa SUMAJKT Energies ili kujionea shughuli za…

  • WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BODI MPYA YA SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji. Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma. Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

  • Shule ya Jitegemee JKT yatimiza miaka 50, Jenerali Mhona atia neno

    Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Oparesheni Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ Meja Jenerali Ibrahim Michael Muhona ameipongeza Shule ya Sekondari Jitegemee JKT kwa kutimiza Miaka 50 Tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza katika Sherehe ya Maadhimisho hayo zilizoambatana na Harambee maalaumu ya kuchangia maboresho ya Shule hiyo Meja Jenerali Muhona amesema JWTZ linaunga mkono dhamira ya Mageuzi inayofanyika, huku akitoa wito kwa walimu kuhakikisha Shule inaendeleza viwango bora vya Ufahulu. Kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Jitegemee JKT kilifanyika tarehe 01 Novemba 2024 ukumbi wa Isamuhyo Mgulani JKT. CHANGIA ELIMU KWA MABORESHO YA MIUNDO MBINU1.NMB….236100419222.CRDB…01508929587003.LIPA….22426113 TIGO.4.LIPA….54359412 VODACOMMajina…

  • MAAFISA JKT WAMEASWA KUTEKELEZA KWA WELEDI JUKUMU LA MALEZI YA VIJANA

    Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana. Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa…

  • Brig. Jen. Ngata awapongeza watendaji SUMAJKT

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT. Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *