KAMISHNA WA JKT KUTOKA NCHINI NAMIBIA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA SUMAJKT
Kamishna wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Namibia Dkt. Felix Masukubili amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Leo tarehe 18 Novemba 2024 Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam. Dkt. Masukubili amepokelewa na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji Kanali Festus Mang’wela. Akiwa katika ziara hiyo amejionea shughuli za uzalishaji Mali zinazofanywa na SUMAJKT ikiwemo kiwanda cha kutengeneza Taa cha SUMAJKT SKYZONE CO.LTD ambacho kinazalisha taa zinazotumia nishati ya jua na umeme, kilichopo Mlalakuwa…


