-
-
SUMAJKT MARATHON YAZINDULIWA
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz Twendezetu Pace ya Kwata Mapigano Na Mwendo
-
Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT awaasa watendaji juu ya vihatarishi
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema, kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa vihatarishi katika utendaji, Shirika limeamua kufanya mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watendaji ili kuwajengea uwezo katika kutambua, kutathimini na kudhibiti vihatarishi kwa lengo la kuleta tija katika utendaji. Brigedia Jenerali Ngata, amezungumza hayo Machi 4, 2026 katika ukumbi wa Umoja unaosimamiwa na SUMAJKT Catering Co.Ltd uliopo Mwenge Dar es Salaam.
-
Mej Jen. Isamuhyo (Mstaafu) aongoza kikao cha bodi SUMAJKT
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Michael Isamuhyo (mstaafu) ameongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT na kufanya ziara ya kutembelea Viwanda vya Shirika ambavyo ni kiwanda cha Viatu na Bidhaa Ngozi, Kiwanda cha Insignia, Kiwanda cha Maji, Kiwanda cha Ushonaji pamoja na kituo cha mafuta SUMAJKT Energies. Ziara hiyo ya Bodi ya Ushauri SUMAJKT kutembelea viwanda imefanyika Machi 5, 2026 jijini Dar es Salaam. Aidha, ziara hiyo ni sehemu ya utambulisho wa shughuli zinazofanywa na Shirika kwa Bodi ya Ushauri Mpya iliyoanza kufanya kikao cha kwanza leo…
-
Brig. Jen. Ngata awapongeza watendaji SUMAJKT
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT. Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.
-
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BODI MPYA YA SUMAJKT
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji. Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma. Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo…


