MAAFISA FANYENI KAZI KWA BIDII, MJIIMARISHE KIUTENDAJI – MEJA JENERALI ( MSTAAFU) MADAWILI
Meja Jenerali (Mstaafu) Zawadi Madawili ametoa wito kwa Maafisa wanawake wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiutendaji katika nafasi zao mbalimbali wanazohudumu. Meja Jenerali Mstaafu Madawili ameyasema hayo tarehe 02 Mei 2025 katika kikao cha Umoja wa Maafisa wa kike wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga (JKT) pamoja na Kamandi nyingine ambacho kimefanyika katika Hoteli ya Ndege Beach Mbweni JKT Jijini Dar es salaam. Aidha ameeleza siri ya kudumu muda mrefu katika Utumishi ni kufuata Misingi iliyowekwa ambayo ni pamoja na Nidhamu katika kazi, roho…


