-
-
Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT amuaga Jenerali Musuguri
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es salaam. Tukio la Kuaga Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) aliyefariki Oktoba 29, 2024 limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango. Viongozi wengine waliohudhuria Tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Maafisa Majenerali, Maafisa…
-
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aongoza waombolezaji kumuaga Meja Jenerali Charles Mbuge
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024. Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu…
-
Buriani Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu)
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wote wa Umma JKT, wanaungana na familia kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT 2019-2021 Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu). Apumzike kwa Amani.


