Brig. Jen. Ngata awapongeza watendaji SUMAJKT

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wa shirika kwa kuzalisha na kutoa huduma bora kupitia Kampuni tanzu za SUMAJKT.

Brigedia Jenerali Ngata, ameongea hayo katika kikao cha tathimini cha shirika kilichofanyika Januari, 16, 2026 katika Ukumbi wa mkutano Makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Chamwino jijini Dodoma.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi, Wakurugenzi Makao Makuu ya Shirika, wakuu wa Kanda za Ujenzi, Kampuni, Miradi na Shule.

Similar Posts

  • CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.

    CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda, amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa maono ya kuanzisha Kampuni ya Bima ya Maisha (SUMAJKT Life Insurance Co. Ltd) itakayokuwa Msaada mkubwa kwa Watanzania kwa Vizazi vya sasa na Vijavyo. Jenerali Mkunda, ameyasema hayo Tarehe 10 Mei 2025 katika Sherehe ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Maisha ya SUMAJKT tukio lililofanyika Ukunbi wa (The Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam. CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Amesema imani yake ni kuona watanzania wakipatiwa huduma hiyo ya Bima kwani Jeshi…

  • WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BODI MPYA YA SUMAJKT

    Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji. Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma. Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo…

  • |

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi

    Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao. Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na  Majeshi ya  nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya…

  • SUMAJKT yatembelewa na Ugeni kutoka Comoros

    Ugeni kutoka Kisiwa cha Comoro, tarehe 06 Septemba 23 umetembelea Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo Mlalakua jijini Dar es salaam. Ujumbe huo wa watu watano ukiongozwa na Mhe. Gavana Sitti Farouata Mhoudine umefika Makao Makuu ya SUMAJKT kwa ziara ya kikazi na umepokelewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Mhe. Gavana Sitti Farouata katika ziara hiyo amepata fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT kupitia Taarifa fupi iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa SUMAJKT. Luteni Kanali George Wang’ombe.Taarifa hiyo…

  • SUMAJKT Kutafuta Fursa za Biashara visiwani Comoro

    Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha…

  • SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *