WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BODI MPYA YA SUMAJKT
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb) ameitaka Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi ya shirika hilo iliyomaliza muda wake kwa kuweka mbele Ubunifu, Mikakati pamoja na kuibua Miradi mipya ya kiuwekezaji.
Mhe. Waziri Rhimo Nyansaho, amezungumza hayo leo tarehe 14 Januari 2026 baada ya kuzindua Bodi Mpya ya Ushauri ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Chamwino jijini Dodoma.





Aidha, Mhe. waziri Nyansaho amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa kwao na kutoa rai kwao kuendelea kusaidia SUMAJKT kusonga mbele na kufikia malengo ya kuanzishwa kwake mwaka 1981.
Bodi mpya ya SUMAJKT itaongozwa na Mwenyekiti Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo, aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri SUMAJKT Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, kumaliza muda wa uongozi.


