WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CDF NA MAKAMANDA WA JWTZ KWA MWAKA 2024

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, amefungua Mkutano wa Nane wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika Ukumbi wa Jenerali Jacob Mkunda uliopo katika Kikosi cha JKT Msange mkoani Tabora leo Desemba 16,2024

Mhe. Dkt. Stergomena Tax amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuendeleza utaratibu wa kufanya kikao hicho kikubwa Jeshini kwa Makamanda, kwani kinatoa fursa ya kutafakari na kushauriana masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Aidha, Mhe. Dkt. Stergomena Tax ameweza pia kuzindua Bwalo la Vijana wa JKT katika Kikosi hicho lililopewa jina la Jenerali Jacob John Mkunda

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *