RUVU JKT WAACHANA NA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA
Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax ameupongeza uongozi wa kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mkoani Pwani kwa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati ya gesi kwa asilimia 100. Ruvu JKT waachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Mhe.Dkt. Tax ametoa pongezi hizo tarehe 3 Aprili 2025 wakati alipofanya ziara kikosini hapo na kujionea namna kikosi hicho chini ya Uongozi wa kamanda kikosi Kanali Peter Mnyani unavyotekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100.
Amepongeza ubunifu wa kuanzisha bustani ya wanayama pori walio wapole na kuwakaribisha watanzania kutembelea bustani hiyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza utalii wa ndani.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube. Ruvu JKT waachana na matumizi ya kuni na mkaa.
https://www.instagram.com/reel/DH_230dOHqP/?igsh=MTdlMTdqOHpubWNwOA==