Kampuni ya usafi SUMAJKT yasaini mkataba na Halmashauri ya Jiji Dar
Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd imetia Saini Mkataba wa kufanya Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Katika Maeneo ya Soko la Buguruni Pamoja na Soko la Ilala leo tarehe18 Februari 2025.
Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Elihuruma Mabelya, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto, Madiwani, na wadau wa Maendeleo imehusisha pia Uzinduzi wa Magari yaliyo nunuliwa na jiji yatakayotumika Katika Usafi.


Akizungumza mara baada ya Kutia Saini Mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo, amesema Serikali ina Imani na Kampuni ya Usafi ya SUMAJKT kwani imekua ikitekeleza Miradi kwa Ufanisi na kwa wakati.
Aidha Mstahiki Meya wa Jiji hilo Mhe. Omary Kumbilamoto, ameeleza kwamba siri ya Kusaini Mkataba huo na SUMAJKT ni utendaji wao wa kazi.
Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd. Kapteni Rosemary Katani, ameeleza kuwa Kampuni hiyo imejipanga Kufanya mapinduzi makubwa katika Usafi.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube