SUMAJKT Electric Co yafikisha umeme Gairo na Kilosa

Kampuni ya Umeme ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT imekamilisha mradi wa Upelekaji Umeme katika Wilaya ya Gairo na Kilosa za Mkoa wa Morogoro.

Mradi wa Upelekaji Umeme katika Vijiji hivyo ni Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita Kupitia wizara ya Nishati ambapo SUMAJKT Electric Co. Ltd. imeshirkiana vyema na Wakala wa Nishaji Vijiji REA katika kuhakikisha Umeme unafika kwa wakati.

Katika wilaya ya Gairo idadi ya vijiji nane ambavyo ni Nongwe, mtega, Lukinga, Mkobwe, Mahelo,, Lufikili, Njungwa,Ikwamba tayari vimepata Umeme.

Aidha katika wilaya ya Kilosa Vijiji vya Mfuluni na Idete navyo tayari vimepata Umeme.

Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT inaendelea Kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo ukamilishwaji wa Mradi wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *