Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wote wa Umma JKT, wanaungana na familia kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT 2019-2021 Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu). Apumzike kwa Amani.
Similar Posts
Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT amuaga Jenerali Musuguri
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, akitoa heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es salaam. Tukio la Kuaga Mwili wa Marehemu Jenerali David Musuguri (Mstaafu) aliyefariki Oktoba 29, 2024 limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango. Viongozi wengine waliohudhuria Tukio hilo ni Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri wa Ulinzi Dkt. Stergomena Tax, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, Maafisa Majenerali, Maafisa…
MAAFISA FANYENI KAZI KWA BIDII, MJIIMARISHE KIUTENDAJI – MEJA JENERALI ( MSTAAFU) MADAWILI
Meja Jenerali (Mstaafu) Zawadi Madawili ametoa wito kwa Maafisa wanawake wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiutendaji katika nafasi zao mbalimbali wanazohudumu. Meja Jenerali Mstaafu Madawili ameyasema hayo tarehe 02 Mei 2025 katika kikao cha Umoja wa Maafisa wa kike wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga (JKT) pamoja na Kamandi nyingine ambacho kimefanyika katika Hoteli ya Ndege Beach Mbweni JKT Jijini Dar es salaam. Aidha ameeleza siri ya kudumu muda mrefu katika Utumishi ni kufuata Misingi iliyowekwa ambayo ni pamoja na Nidhamu katika kazi, roho…
SUMAJKT MARATHON YAZINDULIWA
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz Twendezetu Pace ya Kwata Mapigano Na Mwendo
CDF MKUNDA AKABIDHIWA VIFAA VYA KUKIMBILIA
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, akikabidhiwa vifaa vya kukimbilia (Running Kit) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa ajili ya Kushiriki SUMAJKT Marathon itakayofanyika Tarehe 07 Juni 2026 (Jumapili hii) katika eneo la SUMAJKT House lililopo Medeli East jirani na Taa za Barabarani zilizopo njia panda ya kuelekea kwa Waziri Mkuu Jijini Dodoma. Kupata ratiba nzima ya Marathon gusa link hii hapa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aongoza waombolezaji kumuaga Meja Jenerali Charles Mbuge
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024. Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu…


