SUMAJKT Kutafuta Fursa za Biashara visiwani Comoro

Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi.

Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata.

Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja na Serikali yake ambapo walimueleza shughuli wanazofanya na Sekta wanazoweza kushirikiana ambazo ni ujenzi, Uzalishaji wa bidhaa za chakula na mifugo, Madawa na nguo hususan sare.

Aidha, Shirika la SUMA JKT linatoa huduma za ushauri na usimamizi wa miradi, Utoaji huduma za katika bandari na elimu.

Shirika la SUMA JKT tayari lina soko la bidhaa nchini Comoro ambapo wanasambaza sare za makampuni ya ulinzi nchini humo.

Kwa upande wake, Gavana wa Kisiwa hicho aliushukuru uongozi wa SUMA JKT kwa kuitikia mwaliko wake na kuwasarifu fursa za kuanza ufuatuliaji.

Ujumbe huo unatarajiwa kuwa na mikutano na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro na pia sekta binafsi.

Similar Posts

  • MAAFISA JKT WAMEASWA KUTEKELEZA KWA WELEDI JUKUMU LA MALEZI YA VIJANA

    Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana. Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa…

  • DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

    DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…

  • SUMAJKT yazindua gari kuongeza ufanisi shule ya Kawawa

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amezindua Gari aina ya TATA Marcopolo kwa ajili ya Matumizi ya Shule ya Awali na Msingi ya Kawawa iliyopo Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa. Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Brigedia Jenerali Ngata ameutaka Uongozi wa Shule hiyo kutunza Vitendea kazi vinavyo nunuliwa ikiwemo gari hilo ili viweze kufanya kazi kwa Muda mrefu kwa manufaa ya Shule na Shirika kwa Ujumla. Akitoa taarifa fupi kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Shule ya Kawawa Kanali Ernest Sikaponda amelishukuru shirika kwa kufanikisha Ununuzi wa gari…

  • Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa

    Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika. Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika. Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika…

  • |

    RC CHALAMILA AAGIZA HALMASHAURI ZIFUNGE TAA ZA SUMAJKT

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Albert Chalamila ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zilizopo Dar es Salaam kuhakikisha wanafika kiwanda cha SUMAJKT Skyzone kilichopo Mlalakua jijini hapo ili kutoa oda za kutengeneza taa bora za barabarani. “Tumepita tumeona teknolojia ya kiwanda hiki., naomba nitoe neno rasmi.., wakurugenzi wote wa halmashauri za Dar es Salaam, kufanya ziara mara moja katika kiwanda hiki, na ikiwezekana kutoa oda za taa.., ili ziweze kufungwa kwenye mji wetu kuhakikisha mji unafanya kazi masaa 24.” Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata amesema kwamba Kiwanda hiko ni cha kwanza kabisa kwa aina…

  • Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma

    Mwenyekiti kamati ya NaneNane akaribisha wananchi Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wakulima Nanenane Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Shija Lupi amewakaribisha wananchi wote hapa nchini kutembelea Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma na Kikanda katika Kanda zote ambazo Jeshi hilo linashiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *