Brigedia Jenerali Petro Ngata apokelewa kwa Furaha SUMAJKT

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa Brigedia Jenerali Petro Ngata, amepokelewa kwa furaha na Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT katika ukumbi wa Mikutano, Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

Brigedia Jenerali Ngata akipokelewa kwa mara ya kwanza tangu apandishwe cheo hicho kutoka cheo cha Kanali, alianza kukaribishwa kwa gwaride la heshima na baadae kupokelewa na kamati ya Utendaji ya SUMAJKT.

Akizungumza katika ukumbi wa mikutano Brigedia Jenerali Ngata ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu Meja Jenerali Rajab Mabele kwa kumuamini na kumpatia jukumu la kuendesha Shirika la Uzalishaji Mali katika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata akifurahia jambo na wajumbe wa kamati ya ushauri ya shirika (hawapo pichani).

Aidha amewashukuru Wakurugenzi, wakuu wa Miradi na Watendaji wote wa shirika kuendelea kumpatia Ushirikiano katika kuhakikisha SUMAJKT linatekeleza majukumu yake kwa weledi..

Akitoa shukrani hizo Brigedia Jenerali Ngata amefafanua kuwa ubora wa kazi na huduma zinazotolewa kwenye jamii na SUMAJKT ni ushirikiano mzuri baina yake na watendaji wote wa shirika katika nafasi mbalimbali.

“Katika utekelezaji wa majukumu yangu, siwezi kufanya chochote peke yangu, ipo Miradi mingi kila mwaka inayotekelezwa na Kampuni ya Ujenzi sasa Mkurugenzi hawezi akawa kila mahali, kuna watendaji katika ngazi ya Makao Makuu ambao ndio washauri wangu wa karibu, na ushauri huo umeniwezesha kutoa maelekezo yaliyo sahihi katika miradi yetu na ndio maana tumeweza kufanya vizuri kama Shirika.” Alisema Brigedia Ngata.

Aidha BRIGEDIA Jenerali Ngata, amewapongeza Wakurugenzi, Wakuu wa Miradi na watendaji wote kwa jitihada wanazozionyesha katika kutimiza majukumu kwani Shirika limeendelea kukua na kujitangaza kila kukicha kutokana na weledi wa watendaji.

Akikimkaribisha katika kikao hicho cha kumpongeza Brigedia Jenerali Ngata, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Kanali Robert Kessy, amesema mapokezi hayo yameambatana na furaha za watendaji za watendaji ambao wanajivunia mafanikio hayo.

“Afande tunakupongeza na tuna furaha sana kukuona katika cheo kipya cha Brigedia Jenerali hata nyuso za watendaji zinaakisi furaha itokayo ndani kwenye mioyo, si kingine bali ni baraka ya kupandishwa cheo kwako.” Alisema Kanali Kessy.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Viwanda SUMAJKT Luteni Kanali Leah Mtuma, kwa niaba ya Wakurugenzi wa Shirika amesema wataendelea ushirikiano katika kutimiza majukumu ili kulifanya shirika lizidi kusonga mbele zaidi.

Baada ya kikap hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa ilifuatiwa na hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Uhuru uliopo Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Similar Posts

  • SUMAJKT Kutafuta Fursa za Biashara visiwani Comoro

    Ujumbe wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi. Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata. Mara baada ya kuwasili, Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha…

  • Meja Jen. Mabele aikaribisha SUA Makao Makuu ya JKT Dodoma.

    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa. Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho. Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo…

  • Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja atembelea SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim atembelea SUMAJKT akiangalia Bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata alimpokea Gavana wa Ngazidja Mze Mohamed Ibrahim baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), tarehe 05 Octoba 2024. Ambapo Ugeni huo Ulikuja Tanzania kwa ajili ya Mahusiano ya kibiashara na SUMAJKT. Akiambatana na ujumbe kutoka Comoro, Gavana alipata wasaa wa kutembelea na kujionea bidhaa mbalimbali katika Banda la Maonesho ya Bidhaa na Huduma alipotembelea Makao Makuu ya shirika…

  • Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ

    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu. “Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi…

  • Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT

    Wakufunzi CUJKT watembelea SUMAJKT. Wakufunzi na Maafisa wanaoshiriki Kozi Elekezi kutoka Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) tarehe 18 Machi 2025 wamefanya Ziara ya kimasomo katika Shirika la Uzalishaji la Jeshi la kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa lengo la kuona Shughuli zinazofanywa na Kampuni zake Tanzu zilizopo eneo la Makao Makuu ya Shirika hilo Mlalakuwa na zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo iliyolenga kujifunza kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMAJKT, namna ambavyo huratibiwa na kutekelezwa pamoja na mchango wa Shirika kwa JKT na taifa kwa Ujumla, itaendelea hapo kesho tarehe 19 machi 2025 ambapo Wakufunzi na wanafunzi…

  • GAVANA WA COMORO AVUTIWA NA BIDHAA ZA SUMAJKT

    Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim, ameridhishwa na Huduma na Bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT). Mhe. Mze Ibrahim amebainisha hayo baada ya ziara yake Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es salaam ambayo imelenga kuendeleza Uhusiano wa kibiashara baina ya SUMAJKT na nchi ya Comoro. Katika ziara hiyo Gavana ameambatana na Wakurugenzi wa Chemba ya Biashara kutoka nchini humo, Pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Comoro nchini Tanzania. Baada ya kuwasili Makao Makuu ya SUMAJKT Mhe.Mze Mohammed amepatiwa taarifa kuhusu SUMAJKT ambayo imeainisha maeneo ambayo wanaweza kushirikiana…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *