Brigedia Shija Luppi atembelea SUMAJKT Furniture Showroom

BRIGEDIA SHIJA LUPPI ATEMBELEA SHOWROOM YA SUMAJKT FURNITURE COMPANY

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Shija Lupi, ametembelea Eneo la Mauzo (Show room) la Kampuni ya Samani (SUMAJKT Chang’ombe Furniture Co.Ltd) lililopo karibu na Barabara ya Mwai kibaki Mlalakuwa Jijini Dar es salaam, tarehe 01 Disemba 2025 ili kuona Mwenendo wa biashara unavyoendelea. Brigedia Jenerali Lupi amepokelewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Meja Hemed Mchwanga ambapo amemueleza kuwa Kasi ya wateja kununua Samani zinazozalishwa na Kampuni ya SUMAJKT imeongezeka mara dufu katika kipindi hiki cha mwisho wa Mwaka. Kampuni ya Samani ya SUMAJKT imeendelea kuzalisha bidhaa Bora na za Kisasa za aina mbalimbali na kuwauzia wateja kutoka maeneo tofauti nchini na nje ya nchi. Ofisi kuu za Kampuni hiyo zipo Chang’ombe karibu na Kituo cha Mwendokasi cha Keko wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. @sumajktfurniture Mawasiliano. 0718 803 800 0775 414 307

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *