DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa.

Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi.

Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea na Viongozi pamoja na watendaji wa Miradi hiyo ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri wanazozifanya.

Aidha amewataka kuendelea kuwa wabunifu na kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kufikia malengo yaliyowekwa na Shirika.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *