Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu
Brig. Ngata awataka Wakurugenzi kuongeza Ubunifu. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, amewataka Wakurugenzi waendeshaji wa Viwanda vya Uzalishaji Maji, Ushonaji na Shule ya Sekondari Jitegemee vilivyopo Mgulani JKT kuongeza ubunifu katika Uendeshaji wa Miradi ya kiuchumi na yenye tija kwa Taifa.
Brigedia Jenerali Ngata, amesema hayo Oktoba 03, 2025 alipotembelea viwanda pamoja na shule ya Jitegemee kwa lengo la kuona maendeleo ya viwanda hivyo vilivyopo mgulani JKT jijini Dar es Salaam.





Aidha, Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema Makao Makuu ya Shirika inaendelea kuboresha Viwanda, Kampuni, Miradi na Shule za SUMAJKT ili Shirika lizidi kuimarika ndani na nje ya Tanzania.
https://www.instagram.com/p/DPWnNLBjOcI/?img_index=8&igsh=MWlodmJtbnB0bDl0cg==