Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane

Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amempongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kuboresha Maonesho ya Wakulima Nanenane katika Banda la JKT.

Dkt. Serera ametoa pongezi hizo leo tarehe 6 Agost 2025, alipotembelea Banda la JKT katika Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa Nzuguni Dodoma.

Vilevile, Dkt. Serera amefurahishwa na Ubunifu wa bidhaa zinazozalishwa na Huduma zinazotolewa na JKT pamoja na Shirika lake la SUMAJKT. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane.

Mhe.Serera amepongeza JKT kwa kuendelea kuilinda imani ya Wananchi juu ya Jeshi hilo kwa kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma bora ikiwemo utekelezaji mzuri wa Miradi ya Ujenzi.

Aidha, Dkt. Serera amepongeza JKT kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza Sekta ya Kilimo kwa kuuza Zana bora za Kilimo ikiwemo Pump za umwagiliaji na utekelezaji mzuri wa shughuli za Kilimo, mifugo na Uvuvi. Dkt. Serera ampongeza Mkuu wa JKT kwa ubora wa maonesho ya Nane Nane.

Dkt. Suleiman Serera amepokelewa na Mwenyekiti wa Maonesho Kitaifa JKT Kanali Shija Lupi ambaye alimpitisha katika Banda la JKT kujionea Shughuli zinazofanywa na Jeshi hilo pamoja na Shirika lake SUMAJKT.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *