MKUU WA JKT AMSHUKURU RAIS NA AMIRI JESHI MKUU MAFUNZO YA JKT
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza mafunzo ya vijana wa JKT. Mkuu wa JKT amshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu mafunzo ya JKT.
Meja Jenerali Mabele, ameyasema hayo leo tarehe 17 Aprili 2025 alipokuwa anahitimisha mafunzo ya Awali ya kijeshi kwa vijana wa Operesheni miaka 60 ya Muungano katika kikosi Cha Ruvu JKT kilichopo mlandizi mkoani Pwani.
Amesema Malezi ni suala Mtambuka, yanaanzia ngazi ya familia, Vijana wanapofika makambini. Jeshi la Kujenga Taifa linawafundisha Vijana kuipenda na kuitumikia nchi yao ya Tanzania, linawajengea Uzalendo, Kuwafunza nidhamu, Ukakamavu na Umoja wa Kitaifa ili kijana anapotoka JKT awe Mtiifu, Hodari na Mwaminifu.
Aidha, Meja Jenerali Mabele, amewaasa vijana hao kuzingatia na kutunza Afya zao kwa kipindi chote cha miezi 20 kilichobaki kwani afya ndio msingi na mtaji mkubwa kwa kijana ili awe na sifa za kuchukuliwa na vyombo vya Ulinzi na usalama.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Brigedia Jenerali Abubakar Charo, amewataka kwenda kuzingatia Mafunzo ya Stadi za Kazi na Stadi za Maisha kwani ndiyo yatakayowasaidia kujitegemea baada ya kumaliza mkataba wa Jeshi la Kujenga Taifa.





Kamanda Kikosi Ruvu JKT Kanali Peter Mnyani akitoa taarifa fupi ya mafunzo amesema mafunzo hayo yalianza tarehe 30 Desemba 2024 na kuhitimishwa tarehe tarehe 17 Aprili 2025.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube