VIJANA WAHITIMU JKT WAASWA MATUMIZI MAZURI YA MITANDAO YA KIJAMII

Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Mhe. Williman Kapenjama, amewaasa na kuwakumbusha vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi kundi la Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano juu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii. Vijana wahitimu waaswa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii.

Mhe. Kapenjama, amezungumza hayo leo tarehe 08 Aprili 2025, alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kundi la kujitolea katika kikosi mlale JKT mkoani Ruvuma.

Aidha, amebainisha kuwa vijana wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hivyo hutazama mambo ambayo ni kinyume na tamaduni za kiafrika.

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Brigedia Jenerali Aboubakar Charo, amesema mafunzo ya awali ya kijeshi yanamjenga kijana kuwa tayari kujifunza mafunzo mengine ya stadi za maisha na kazi ambapo kijana atakuwa na nidhamu, ukakamavu, uzalendo, uhodari, uvumilivu, kujiamini na moyo wa kupenda kufanya kazi. Vijana wahitimu waaswa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii

Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT Kanali Longinus Nyingo, amesema mafunzo ya awali ya kijeshi JKT ni muendelezo wa utekelezaji wa mawazo ya muasisi wa Taifa la Tanzania Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika uanzishwaji wa JKT.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
https://www.instagram.com/p/DIL5WkIo_1Q/?igsh=c2ViaWhscHB6ZXR1

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *