MAAFISA JKT WAMEASWA KUTEKELEZA KWA WELEDI JUKUMU LA MALEZI YA VIJANA

Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana. Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amewaasa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutekeleza kwa weledi jukumu la Malezi ya Vijana.

Kanali Mrai ametoa rai hiyo tarehe 21 Machi 2025 wakati akihitimisha Semina Elekezi ya Maafisa wa JWTZ waliopewa Uhamisho kwenda JKT, iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (CUJKT) kilichopo Kimbiji Jijini Dar es Salaam

Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiendesha Semina Elekezi kwa watendaji wake ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu ya JKT ambayo ni Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi. Maafsa JKT wameaswa kutekeleza kwa weledi jukumu la malezi ya vijana.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube


chanzo: https://www.instagram.com/reel/DHfax_8IKgt/?igsh=b3UxNngwcXFzZ256

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *