Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika leo tarehe 14 Machi 2025 katika ukumbi wa Mebele jijini Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kupitisha makadirio ya bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Kikao hicho cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT kimehudhuriwa na Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Wajumbe wa Bodi na wajumbe waalikwa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na SUMAJKT. Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu) aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *