Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda

Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda. Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amefunga Kikao cha Wakuu wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo tarehe 26 Feb 2025  katika hoteli ya Girrafe jijini Dar es Salaam.

Luteni Jenerali Salum Othman, amesema Mkutano huo huibua fursa, Masoko  na namna nzuri ya kuboresha teknolojia  ya Viwanda na Mashirika ya jumuiya hiyo. Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda.

Akizungumza kuhusu lengo la Mkutano huo, ameeleza ni kuweka pamoja  na kuimarisha ushirikiano wa Mashirika na Viwanda vinavyomilikiwa  na Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Kikao cha Wakuu wa Viwanda na Mashirika ya Kijeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye ni Mkuu wa Shirika la Nyumbu Brigedia Jenerali Seif Hamis, amesema kikao hicho hufanyika  nchi moja hadi nyingine ambapo  kwa mwaka huu kimefanyika Tanzania na mwakani kitafanyika nchini Rwanda.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema Wakuu wa Mashirika  na Viwanda wa Jumuiya hiyo  wamevutiwa na bidhaa zinazozalishwa  na Jeshi la Ulinzi Tanzania. Mnadhimu Mkuu afunga kikao cha Wakuu wa Viwanda.

Awali kabla ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salumu Haji Othman, kufunga mkutano wajumbe walitembelea Kiwanda cha Taa cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd na Maonesho maalumu ya bidhaa za Viwanda vya Mashirika ya Jeshi la Ulinzi Tanzania ambayo ni  SUMAJKT, MZINGA na NYUMBU katika viwanja vya TPDF Lugalo Golf Club.

Mkutano huo ambao ni wa watatu kufanyika pamoja na maonesho tangu kuanzishwa kwake unalenga kuonesha fursa zilizopo kwa kila nchi mwanachama katika eneo la malighafi, vipuri na bidhaa zilizokamilika ili ziweze kupata Masoko ndani ya ukunda kwa nchi wanachama wa kabla ya kuziuza nje ya ukanda na mabara mengine ili kujipatia kipato na kujijengea uchumi tegemevu.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *