Waziri Kabudi aridhishwa na Ujenzi wa viwanja kwa ajili ya CHAN.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Kabudi (Mb) ameridhishwa na kazi inayofanywa na Kampuni ya SUMAJKT Construction Company Ltd, katika ujenzi wa viwanja vya mazoezi kwa ajili michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) yatakayofanyika mwezi Februari mwaka 2025.
Katika Ukaguzi huo Profesa Kabudi, amefafanua kwamba viwanja hivyo vitakamilika ifikapo tarehe 21 Januari 2025 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa mazoezi ya michuano ya CHAN.
Nae Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, kwa niaba JWTZ ameeleza kwamba JKT limekabidhiwa kazi hivyo litaitekeleza kazi hiyo kwa muda uliopangwa.
Aidha katika ziara hiyo Profesa Kabudi, ameongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Methusela Ntoda, Rais wa TFF Rais Wallace Karia, Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu – CHAN Salum Madadi.
Katika Ziara hiyo, Profesa Kabudi ametembelea Kiwanja cha Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni, Shule ya Sheria Tanzania na Gymkhana Football Club.
Habari zaidi tazama video hii hapa chini..