Brig. Ngata akagua maandalizi Gymkhana
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, tarehe 14 Novemba 2024 amekagua maandalizi ya ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu Gymkhana Dar es Salaam kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) itakayofanyika mwaka 2027.
Katika Ukaguzi huo Brigedia Jenerali Ngata, ameongozana na Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu Shirikisho la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) Salum Madadi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi SUMAJKT Mhandisi Morgan Nyonyi na Kapteni wa Gymkhana Football Club, Bw. Saleh Geva.