JESHI la Kujenga Taifa (JKT) latangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujitolea kwa mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo huku watakaopata nafasi hizo wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Novemba 1 hadi 3 Mwaka huu. Akizungumza Septemba 25, 2024 na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT,Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Kanali Juma Mrai amesema usaili utaanza Oktoba 1, mwaka huu kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar. “Mkuu wa Jeshi…


