Kampuni ya usafi SUMAJKT yasaini mkataba na Halmashauri ya Jiji Dar
Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd imetia Saini Mkataba wa kufanya Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Katika Maeneo ya Soko la Buguruni Pamoja na Soko la Ilala leo tarehe18 Februari 2025. Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Elihuruma Mabelya, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto, Madiwani, na wadau wa Maendeleo imehusisha pia Uzinduzi wa Magari yaliyo nunuliwa na jiji yatakayotumika Katika Usafi. Akizungumza mara baada ya Kutia Saini Mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo,…


