VIJANA WAHITIMU JKT WAASWA MATUMIZI MAZURI YA MITANDAO YA KIJAMII
Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Mhe. Williman Kapenjama, amewaasa na kuwakumbusha vijana wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi kundi la Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano juu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii. Vijana wahitimu waaswa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mhe. Kapenjama, amezungumza hayo leo tarehe 08 Aprili 2025, alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa kundi la kujitolea katika kikosi mlale JKT mkoani Ruvuma. Aidha, amebainisha kuwa vijana wengi hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii hivyo hutazama mambo ambayo ni kinyume na tamaduni za kiafrika. Nae Mwakilishi…


