Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata, kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema, kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa vihatarishi katika utendaji, Shirika limeamua kufanya mafunzo ya usimamizi wa vihatarishi kwa watendaji ili kuwajengea uwezo katika kutambua, kutathimini na kudhibiti vihatarishi kwa lengo la kuleta tija katika utendaji.

Brigedia Jenerali Ngata, amezungumza hayo Machi 4, 2026 katika ukumbi wa Umoja unaosimamiwa na SUMAJKT Catering Co.Ltd uliopo Mwenge Dar es Salaam.


