SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba

SUMAJKT Yatwaa tuzo Sabasaba. Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limeibuka mshindi wa Kwanza katika Samani na Ubunifu wa ndani katika Maonyesho ya 49 ya Biashara Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dara es Salaam.

Tuzo ya Ushindi huo imekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Selemani Jafo, kwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, katika ufunguzi wa Maonesho hayo leo tarehe 7 Julai 2025 katika Viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia Ushindi huo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, ametoa rai kwa Watanzania na wadau mbalimbali kutembelea Banda la JKT katika maonesho hayo.

JKT limekuwa likishinda katika nyanja tofauti kwenye Maonyesho hayo ambayo ufanyika kila Mwaka.

Maonesho ya 49 ya Biashara kimataifa yamefunguliwa leo rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *