Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT

Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amepokea ugeni wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka nchini Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi, ambaye amefanya ziara Makao Makuu ya SUMAJKT ili kubadilishana uzoefu katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo.

Ugeni huo baaba ya kupokelewa leo tarehe 28 Aprili 2025 umetembelea Kiwanda cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi na Mradi wa SUMAJKT Energies ili kujionea shughuli za kiuchumi zinazofanywa na SUMAJKT.

Ziara hiyo itaendelea kesho ambapo itatembelea Kiwanda cha Maji SUMAJKT Bottling Co.Ltd na Kiwanda cha Nguo SUMAJKT Garment Co.Ltd vilivyopo JKT Mgulani. Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia Shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) limekuwa likipokea ugeni mbalimbali ili kujifunza Shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Shirika hilo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *