Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ, kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kwa kipindi cha robo mwaka kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika katika viunga vya Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma, Jenerali Mkunda amesema mafanikio hayo si ya kawaida kwani yamebeba thamani ya mazoezi, nidhamu, mafunzo, na mshikamano wa Kijeshi, ambapo sasa wanashuhudia ushindi kutoka michezo ya ngumi, riadha, mpira wa mikono, mpira wa magongo na mpira wa kikapu.
“Tumeshuhudia medali, vikombe, tuzo, na hata ushindi wa uongozi wa Kimataifa kupitia Meja Mohamed Kasui kwa kuchaguliwa kuwa wa kwanza kutoka Afrika tangu mwaka 1948 kuwa Rais wa Kamati ya Kikapu ya Kijeshi Duniani , jambo la kihistoria kwa Tanzania na Afrika”, amesema Jenerali Mkunda



Naye Mkuu wa Operesheni na Utendaji Kivita Jeshini Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema wanamichezo wote waliofanikiwa wameonesha kuwa askari wa JWTZ wanaweza kuwa shujaa ndani ya uwanja wa vita na uwanja wa michezo. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewapongeza wanamichezo wa JWTZ.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
https://www.instagram.com/p/DIHNoSIIeOh/?igsh=MWlvM29jeGUwMWNvMQ==