Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameitaka Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT), Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameitaka Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi vinavyonunuliwa ili viweze kudumu na kuleta tija kwa Shirika.
Amezungumza hayo Tarehe 14 Februari 2025, baada ya kufanya Uzinduzi wa Gari Jipya la utawala lililonunuliwa na Kampuni hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi.

Awali akitoa taarifa fupi ya ununuzi wa gari hilo Mkurugenzi Mwendeshaji wa SUMAJKT Electric Co Ltd. Meja James Mhame, amesema kuongezeka kwa gari hilo kutarahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
SUMAJKT Electric Co.Ltd Inajishughulisha na Kandarasi mbalimbali za Miundombinu ya Umeme wa njia ndogo na Kati pamoja na uwekaji Umeme katika Majengo binafsi, Taasisi za Umma na Mashirika.Brigedia Jenerali Petro Ngata Ameisisitiza Kampuni ya Umeme ya SUMAJKT Electric Co Ltd kuvitunza vitendea kazi hivyo.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube