Marehemu Meja Jenerali Busungu azikwa Luchelele Mwanza

Waziri Wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Mhe. Stargomena Lawrence Tax, ameongoza Maafisa, Askari, Vijana, Watumishi wa Umma na Waombolezaji katika Mazishi ya Mwili Wa Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika katika Kijiji Cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Desemba 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, katika Mazishi hayo Mkuu wa Jeshi La Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema Marehemu Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) enzi za uhai wake akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ametumikia Jeshi kwa kipindi cha miaka thelathini na nne (34) alikuwa Mwaminifu, Mtiifu na Hodari katika kutekeleza Majukumu yake.

Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) alifariki Dunia tarehe 24 Desemba 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *