Similar Posts
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aongoza waombolezaji kumuaga Meja Jenerali Charles Mbuge
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024. Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu…
MAAFISA FANYENI KAZI KWA BIDII, MJIIMARISHE KIUTENDAJI – MEJA JENERALI ( MSTAAFU) MADAWILI
Meja Jenerali (Mstaafu) Zawadi Madawili ametoa wito kwa Maafisa wanawake wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiutendaji katika nafasi zao mbalimbali wanazohudumu. Meja Jenerali Mstaafu Madawili ameyasema hayo tarehe 02 Mei 2025 katika kikao cha Umoja wa Maafisa wa kike wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaofanyia kazi Jeshi la Kujenga (JKT) pamoja na Kamandi nyingine ambacho kimefanyika katika Hoteli ya Ndege Beach Mbweni JKT Jijini Dar es salaam. Aidha ameeleza siri ya kudumu muda mrefu katika Utumishi ni kufuata Misingi iliyowekwa ambayo ni pamoja na Nidhamu katika kazi, roho…
Kusitishwa kwa mafunzo ya JKT kulileta athari kubwa ikiwemo ya mmomonyoko wa maadili
” KUSITISHWA KWA MAFUNZO YA JKT KULILETA ATHARI KUBWA IKIWEMO YA MMOMONYOKO WA MAADILI”Wakuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (Wastaafu)Meja Jenerali Martin Madata (Mstaafu) na Meja Jenerali Samwel Kitundu (Mstaafu), wakielezea umuhimu wa Mafunzo ya JKT, athari zilizopatikana baada ya kusitishwa kwa Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na Kujitolea pamoja na Mafanikio yaliyopatikana Baada ya kurejeshwa kwa Mafunzo hayo. Wameyasema hayo wakati wa Mahojiano Maalumu ya Mafanikio yaliyopatikana ndani ya JKT kwa kipindi cha Miaka 60 ya Uwepo wake nchini.https://www.instagram.com/reel/DGvnVdetkhE/?igsh=ZmJua2s1NWlvcndw Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
Buriani Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu)
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Maafisa, Askari, Vijana na watumishi wote wa Umma JKT, wanaungana na familia kuomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT 2019-2021 Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu). Apumzike kwa Amani.
SUMAJKT MARATHON YAZINDULIWA
Usajili wa SUMAJKT MARATHON, Sunday 7 June 2026 UMEFUNGULIWA RASMI na CEO wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kwa kushirikiana na CRDB Bank.JISAJILI KUPITIA TOVUTI YA www.sumajktmarathon.co.tz Twendezetu Pace ya Kwata Mapigano Na Mwendo
Marehemu Meja Jenerali Busungu azikwa Luchelele Mwanza
Waziri Wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Mhe. Stargomena Lawrence Tax, ameongoza Maafisa, Askari, Vijana, Watumishi wa Umma na Waombolezaji katika Mazishi ya Mwili Wa Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika katika Kijiji Cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Desemba 2024. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, katika Mazishi hayo Mkuu wa Jeshi La Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema Marehemu Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) enzi za uhai wake akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ametumikia Jeshi kwa kipindi…


