Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT
Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu Nchini Namibia Meja jenerali Aktofel Nambahu Amevutiwa na Shughuli za Uzalishaji mali zinazofanya na Jeshi la Kujenga Taifa Kupitia Shirika lake SUMAJKT.
Meja Jenerali Nambahu amepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Shija Lupi kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele leo tarehe 20 Agosti 2025 Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Jijini Dar es salaam. Mkuu wa Jeshi Namibia avutiwa na shughuli za SUMAJKT.





Ziara yangu JKT ni mualiko wa Mkuu wa kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu Meja Jenerali Fadhili Nondo na tumepata kujua Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na Shirika lake, pia kiwanda hiki cha maji tulichotembelea leo, tumeona ni kwa namna gani kinahudumia serikali na taasisi mbalimbali, ukizingatia Tanzania ni Moja ya Nchi Mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC hii inaonesha dhahiri kuwa shirika hili linachangia Ukuaji wa Uchumi.